Friday , 28th May , 2021

Mbunge wa Bunda Vijijini Peter Mwita Getere, ameelezea hofu yake ya wanyamapori aina ya Tembo kuongezeka na kwamba siku zinavyozidi kwenda nchi itabaki kuwa ni ya wanyamapori ukizingatia Tembo wenyewe hawana uzazi wa mpango.

Mbunge wa Bunda Vijijini Peter Mwita Getere

Kauli hiyo ameitoa leo Mei 28, 2021, Bungeni Jijini Dodoma wakati akiuliza swali lake kwa Wizara ya Maliasilia alipotaka kujua idadi ya Tembo wanaopaswa kuishi kwenye mapori ya Tanzania.

"Haya mambo ya wanyamapori mimi naona sasa tunakokwenda tutabakiza nchi ya wanyamapori, najiuliza hivi ni Tembo wangapi wanatosha kuishi katika mapori ya Tanzania ambao watalii watakuja kuona kama Tembo hawa hawana uzazi wa mpango," ameuliza Mbunge Getere.