Thursday , 27th May , 2021

Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, amesema miaka 60 tangu uhuru bado Tanzania ina matatizo makubwa ikiwemo eneo la umasikini kwani Watanzania wengi ni maskini.

Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo, Jaji Mstaafu Joseph Warioba

Akizungumza katika Kumbukizi ya Hayati, Edward Moringe Sokoine, Jaji Warioba amesema yeye pamoja na wazee wengi watawaungana mkono Rais na Makamu wa Rais wa Tanzania na kuwapa shauri pale watapohitaji ushauri.

“Tulipopata uhuru tulijiwekea malengo ili tupate maendeleo ni lazima tupige vita ujinga, maradhi na umaskini, katika miaka 60 tangu uhuru nchi imepiga hatua kubwa mpaka kuingia kwenye uchumi wa kati lakini bado tuna matatizo makubwa hasa katika eneo la umaskini,” amesema Jaji Warioba.

Aidha, ameongeza, “Wakulima, wafugaji na wavuvi ndio walio wengi maskini, ni lazima tuinue maisha ya wakulima, wakulima ndio nguzo ya taifa wanafanya kazi kubwa lakini tusijivunie wanatuletea usalama wa chakula wakati wanaendelea kuwa maskini,” amesema Jaji Warioba.