Monday , 24th May , 2021

Muandishi wa Habari kutoka East Africa TV Oliver Nyeriga na wasanii wa BongoFleva Nandy, Harmonize, Idris Sultan, Monalisa wameteuliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo kuwa Mabalozi wa Uhamasishaji Utunzaji wa Mazingira Nchini.

Kutoka kulia ni Muandishi wa Habari wa East Africa TV Oliver Nyeriga, Nandy, Harmonize na Idris Sultan

Waziri Jafo amewateuwa wasanii hao akiwa Jijini Dodoma kwa kusema Mabalozi hao wameteuliwa kutokana na ushawishi wao kwa jamii ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira na upandaji miti.

Aidha mabalozi wengine walioteuliwa na Waziri Jafo ni Afisa Habari wa Klabu ya Simba Haji Manara, Mbunge Esther Matiko, Mbunge Joseph Musukuma, Diamond Platnumz, Sakina Abdulmasoud na mchekeshaji Mai Zumo.