
Msanii Kinata Mc
Wimbo huo ameshirikiana na Ibraah kutoka Konde Music Worldwide ulianza kupata umaarufu kupitia kipande cha video kwenye mitandao ya kijamii na umeendelea kutengeneza rekodi mpya kwake kwani mpaka sasa unashika namba 3 kwenye Trending for music huko YouTube.
Kinata ameonesha uwezo wa kuimba kwa lugha ya kiingereza na kiswahili kwenye mdundo wa singeli kwa lengo la kutanua wigo wa soko lake.