Friday , 28th Nov , 2014

Bondia anayeshikilia uzito wa Super feather wa Kilo 59,Amosi Mwamakula amewataka mabondia hapa nc

Bondia Amosi Mwamakula

Bondia anayeshikilia uzito wa Super feather wa Kilo 59,Amosi Mwamakula amewataka mabondia hapa nchini kuwekeza katika mchezo huo ili kuweza kupata wadhamini kwa ajili ya kukuza mchezo huo.

Akizungumza na East Africa Radio,Mwamakula anayefanyia kazi zake nchini Brazil amesema mabondia wa Tanzania hutgemea mazoezi kipindi cha pambano suala linalokuwa gumu kuweza kufanya vizuri katika mapambano mbalimbali makubwa.

Mwamakula amesema wadhamini huwawezesha mabondia wanaqojali na kuzithamini kazi zao,hivyo kama mabondia hao hawataweza kufanya kazi kwa bidii wasitegemee kupata wadhamini watakaowawezesha kushiriki mapambanoi mbalimbali makubwa na kuweza kufanya vizuri.