Friday , 21st Nov , 2014

Mamlaka ya Mapato Tanzania imesema kuwa inakusidia kuongeza ufanisi wa ukusanyaji kodi hadi kufikia makusanyo ya shilingi trilioni 11.3 mwaka huu.

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Tanzania Shamsi Vuai Nahodha

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Tanzania Shamsi Vuai Nahodha ameitaka Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini Tanzania TRA kuondoa urasimu katika mchakato wa Ukusanyaji wa Kodi na kupunguza wingi wa kodi ili kurahisisha mamlaka hiyo kukusanya kodi ili kufikia malengo na kuiwezesha nchi kupata mapato mengi.

Nahodha ametoa kauli hiyo katika maahimisho ya siku ya Mlipa kodi na kuainisha kuwa ni lazima Serikali ihakikishe huduma muhimu kama dawa katika hospitali,madawati mashuleni,maji na umeme vinapatikana kwa uhakika ili kuonyesha thamani ya kodi ya wananchi na kuwahamasisha watu kulipa kodi.

Kituo cha Television cha ITV kimeshinda tuzo kwa vyombo vya Habari ,wakati Vodacom imeshinda kati ya makampuni ya simu, TBL na TDL vimeshinda kwa makampuni ya vinjwaji na NMB imeshindwa katika sekta ya Mabenki.

TRA imesema inakusidia kuongeza ufanisi wa ukusanyaji kodi hadi kufikia makusanyo ya shilingi trilioni 11.3 mwaka huu.

Wakati huo huo, shirika la viwango nchini Tanzania TBS limewataka wafanyabiashara wadogo na wakubwa nchini kuhakikisha wanazalisha bidhaa ambazo zinahimili soko la ndani na la kimataifa.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya viwanda barani Afrika, Afisa udhibiti na ubora wa TBS Bw. Donald Manyama amesema wafanyabiashara wengi wa Tanzania wanashindwa kuhimili soko la kimataifa kutokana na kutokuwa na ubora wa bidhaa zao.

Tags: