Wednesday , 12th Nov , 2014

Amini, staa ambaye anarejea katika muziki kwa kishindo na mabadiliko makubwa akiwa chini ya usimamizi mkubwa, amesema kuwa safari hii ameamua kuuchukua muziki wa kitanzania wa Mchiriku kwaajili ya kufikisha ujumbe wake kwa mashabiki.

msanii wa bongofleva Amini

Amini ambaye wiki hii anaachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina Mbeleko, amesema kuwa miziki mingi ya sasa hivi inakuwa ni ya kuiga mahadhi ya nnje, tofauti na yeye ambaye ameamua kurudi nyumbani zaidi na kuchagua ladha ambayo inaeleweka na watu wengi katika ngazi mbalimbali za kimaisha.