Wednesday , 9th Dec , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amemtaka Waziri mpya wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa kuhakikisha sekta ya michezo inapiga hatua ikiwemo timu ya taifa kuachana na utamadunia wa Simba na Yanga.

Rais Magufuli kwenye picha kubwa na picha ndogo ni kikosi cha Taifa Stars

Magufuli ametoa kauli hiyo leo Desemba 9, 2020 wakati akiapisha Mawaziri katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa wakati umefika kuachana na mazoea ya vilabu vya Simba na Yanga.

''Wizara ya Michezo tumekupeleka Bashungwa ili tukacheze kweli, tumekupeleka huko tunataka tukashinde kweli, tukienda kucheza tukafungwa sijui magoli 10 mtaondoka wote Waziri  na Naibu Waziri'' - Dkt. Magufuli

Magufuli ameongeza kuwa, ''Tunataka tuwe na timu ya taifa inayoshinda na mambo ya kwenda na Simba na Yanga tu tumechoka inawezakana umefika wakati tuwe na timu ya taifa ambayo haina uhusiano na Simba na Yanga''.