Sunday , 1st Nov , 2020

Winga wa Yanga, Farid Musa amempigia chapuo mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi, kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mchezo kati ya Biashara United dhidi ya Yanga.

Kutoka kushoto ni Farid Mussa, Ditram Nchimbi na Michael Sarpong

Farid Mussa pamoja na mshambuliaji Michael Sarpong na Ditram Nchimbi ndio wametajwa kushindania tuzo hiyo ambayo hupigiwa kura na mashabiki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram klabu ya Yanga imeweka wachezaji hao na kuwataka mashabiki wapige kura na katika moja ya 'comment' Farid Mussa amesema Nchimbi anastahili.

Farid ameandika Nchini duma akamalizia na emoji inayoonesha kumpigia saluti.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume Musoma, Mara Yanga ilishinda goli 1-0 lililofungwa na Michael Sarpong.