Wednesday , 5th Nov , 2014

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo amewataka viongozi wa Soka nchini kuwachukulia hatua kali wachezaji wanaodanganya umri wao katika soka.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Thadeo amesema suala la kudanganya umri ni changamoto inayopelekea kushindwa kupata timu bora ya vijana na hata timu itakayoweza kufanya vizuri baadaye katika mashindano mbalimbali kwa ndani na nje ya nchi.

Thadeo amesema mchezaji anapodanganya umri wake, anazuia wachezaji wenye umri unaostahili kushindwa kuonesha vipaji vyao katika soka hapa nchini.