
Timu ya Tanzania Prisons katika picha ya pamoja
Kazumba ameyasema hayo leo Oktoba 20, 2020 kwenye mahojiano na kipindi cha Kipenga cha East Africa Radio.
''Kikosi chetu kipo sawa sana kwa sasa, tunajiamini tunaweza kupata matokeo katika kiwanja chochote Tanzania hii, hata jana wakati tunacheza na JKT Tanzania bila mapungufu ya mwamuzi alipotoa mkwaju wa penati, basi tungeibuka na ushindi''
Ameongeza kuwa, ''Tanzania Prison na Simba siku zote ni mchezo mgumu sana tangu mimi nacheza timu hii, ndiyo maana hata msimu uliopita pamoja na Simba kutwaa ubingwa wa ligi kuu, lakini hakupata ushindi katika michezo yetu yote miwili na kuambulia alama mbili tu''alisema Kazumba.
Katika ligi ya msimu huu hadi sasa Prisons ina alama 6 baada ya kushuka dimbani mara 6, ikiwa na magoli ya kufunga 4, huku wakiruhusu kufungwa magoli 5. Simba yenyewe imeshuka dimbani mara 5 ina alama 13 ikiwa imefunga magoli 14 huku ikiruhusu magoli 2 tu.