Sunday , 4th Oct , 2020

Rais wa TFF Wallace Karia amesema moja ya changamoto kubwa katika upashaji wa taarifa katika vilabu vya Tanzania, ni suala la idara za habari kutokana na uwepo wa wahamasishaji na sio maafisa habari.

Rais wa TFF Wallace Karia

Ameyasema hayo leo Oktoba 4, 2020 kwenye mkutano wake na wahariri wa habari za michezo Tanzania, ambapo ameeleza kuwa wanaandaa muongozo ambao utasaidia idara hizo kufanya kazi zake kwa weledi.

"Kwa asilimia kubwa Tanzania hatuna maafisa wa habari tuna wahamasishaji, watu wanaongea vitu kutoka kichwani mwao, Afisa Habari anatakiwa kutoa taarifa zilizotolewa na taasisi, kwetu tuna hiyo changamoto, sasa tunaandaa miongozo", amesema Wallace Karia.

Aidha kwa upande mwingine Karia ameongelea suala la timu kupunguzwa kwenye ligi ku soka Tanzania bara ambao amesema suala hilo lilijadiliwa na kutolewa maoni na wadhamini, wadau pamoja na wana habari ili kuboresha ligi.