Wednesday , 30th Sep , 2020

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Chakula Bora, Oddo Ramadhani, amesema wakazi na wananchi mbalimbali wanagongwa na vyombo vya moto katika barabara hiyo kutokana na kukosekana kwa alama za barabarani pamoja na matuta.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Chakula Bora, Oddo Ramadhani.

Akiongea na EATV leo mwenyekiti huyo amesema kwa sasa wazazi wanaogopa kuwatuma watoto wao dukani kwa hofu ya kugongwa na gari au bodaboda kutoka na ukosefu huo wa alama za usalama barabarani ikiwemo matuta.

“Kwa kweli tunaiomba serikali itusaidie katika hili kwa kuwa wananchi wamekuwa na hofu sana wanapopita katika barabara hii” amesema Oddo.

Mwenyekiti huyo wa mtaa amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuitengeza barabara hiyo lakini changamoto kubwa ni ya ajali zinazotokana na kukosekana alama za barabarani ikiwemo matuta ambayo yatafanya vyombo vya moto vipunguze mwendo.