Friday , 25th Sep , 2020

Kiungo mshambuliaji wa PSG Angel Di Maria amemjia juu kocha wa timu ya Taifa
ya Argentina Lionel Scaloni, kwa kutomjumuisha katika kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina kinachojianda kwa michezo miwili dhidi ya Ecuador na Bolivia mwezi ujao.

Angel Di Maria akishangilia moja ya magoli aliyowaifungia timu ya Taifa ya Argentina

''Hajaniita katika kikosi, kwa sababu hanipendi tu, nipo katika kiwango bora kwa sasa nimetoa mchango mkubwa kwa timu yangu katika msimu uliyomalizika, tumetwaa ubingwa wa Ufaransa na tumecheza fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, nikitoa mchango mkubwa kwenye mafanikio hayo, kutonijumuisha kikosini hakunikatishi tamaa, nitapambana nirejee katika kikosi''

Kocha wa Argentina Lionel Scaloni alisema, ataanza kujenga timu mpya ya Taifa kwa kutumia vijana zaidi kwa kuwa asilimia kubwa wachezaji wake wa sasa wamefikisha umri wa juu ya miaka 30 akiwemo Lionel Messi 33 Sergio Kun Aguero 32 na Nicolas Otamendi 32 lakini bado wamejumuishwa hali inayomfanya Di Maria aamini kuwa kocha hampendi

UMUHIMU WA DI MARIA KATIKA TIMU YA TAIFA

Uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja, kuna muda anaweza kucheza kama kiungo wa pembeni ( winga) lakini kuna muda anacheza kama kiungo mchezeshaji wa kati ,pia anauwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa kati, akiwa na timu ya Taifa aliyoanza kuitumikia mwaka 2008 ameichezea mechi 102 na kuifungia magoli 20