Friday , 25th Sep , 2020

Afisa Utumishi mkoa wa Katavi, Clesensia Joseph, amesema kuwa mkoa huo unakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi 242 hali inayolazimu baadhi yao kufanya kazi ambazo hawana taaluma nazo.

Afisa utumishi mkoa wa Katavi Clesensia Joseph

Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi wa sekretarieti ya mkoa yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya mwajiri na mwajiriwa.

"Wachache waliopo wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba malengo yote yanatekelezwa ni athari ya mtu mmoja mmoja kufanya kazi za ziada, imetoa pia fursa ya watumishi wachache waliopo kuweza kujifunza taaluma nyinginezo, kwa sababu unafanya kazi zako na nyingine kadri utakavyopangiwa ili kutekeleza malengo ya taasisi", amesema Clesensia.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi wa baraza hilo, Jamila Kimaro, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mpanda, ametoa miezi 3 kwa wakurugenzi  kuhakikisha wanafufua mabaraza ya wafanyakazi katika halmashauri zao.