
Staa wa LA Lakers, LeBron James(Kulia) na Giannis Atetokounmpo wa Milwaukee Bucks(Kushoto) wakiwa kibaruani
Silver ametoa kauli hiyo kutokana na uwezekano wa muingiliano wa ratiba hizo mbili ambapo Silver amenukuliwa akisema msimu wa NBA hautokuwa tena mwezi Disemba badala yake utaanza mwezi Januari 2021 hii inamaanisha hatua ya mtoano itaisha ndani ya mwezi Agosti au Septemba
Michuano ya Olympic hukusanya wachezaji wa ligi mbalimbali duniani ikiwemo NBA ambao huwakilisha mataifa yao
Aidha Silver amesema nyota 15 bora wa NBA huweza wasishiriki michuano ya Olympic ingawa wengine waliosalia wataendelea kuwakilisha mataiafa yao
Ratiba ya shughuli mbalimbali duniani ikiwemo michezo imeathiriwa kwa kiwango kikubwa hii ni kufuatia dunia kukumbwa na janga la CORONA.