
Watuhumiwwa wa kesi ya uhujumu uchumi
Washtakiwa kàtika kesi hiyo ni Abdulrahman Njozi, Amiri Kapera, James Oigo, Hellen Peter,Ivonne Kimaro, Restiana Lukwalo,Jamira Vulu, Tikyeba Alphonce na Dominic Mbwete.
Uamuzi huo umetolewa hii leo na Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Isaya ambapo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon, na kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika na kesi hiyo Imeahirisha hadi Oktoba 6,mwaka huu.
Awali upande wa utetezi uliowakilishwa na Captain Bendera ulidai kupinga kuahirishwa kwa kesi mara kwa mara bila sababu za msingi.
Aidha Hakimu Isaya amedai kuwa kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi na kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo ambapo pia ameutaka upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi ili haki za washtakiwa zifanyike haraka.
Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matano likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya sh bilioni 2 wanayodaiwa kutenda katika tarehe zisizofahamika kati ya Julai mosi mwaka 2016 hadi Septemba 4 mwaka 2017 jijini Dar es Salaam.