
Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu.
Akizungumza leo Septemba 21, 2020 na wananchi wa Rungwe katika mkutano wake wa kampeni amesema fedha zilizokuwa zikitengwa na halmashauri zimekuwa zikutumiwa na madiwani kujiweka vizuri.
"Mfuko huu ulikuwa unatumika kama mfuko wa kisiasa na
madiwani, walikuwa wanautumia kujiweka vizuri kwenye maeneo yao na kwa maana hiyo fedha hizi zilikuwa hazilipwi na mikopo hii ni mikopo bila riba” alisema Mama Samia
Aidha Mama Samia amesema kuwa lengo la kuundwa kwa mfuko ilikuwa nikuviwezesha vikundi kwa kuwapa fedha ili waweze kufanya biashara
"Lengo la mfuko huu, lengo la hii asilimia kutafuta vikundi vilivyokuwa vimekaa vizuri muwape pesa yakutosha waweze kufanya biashara wajiajiri na waajiri wenzao” alisema Mama Samia