Maafisa waliostaafu kwa vyeo vyao ni wa ngazi ya Luteni Jenerali mmoja, Meja Jenerali maafisa sita pamoja na Brigedia Jenerali maafisa tisa.
Akizungumza baada ya gwaride hilo la heshima Luten General mstaafu Paul Masao ametoa ushauri kwa vijana wanaodhani jeshi ni sehemu ya ajira na kutekeleza matakwa yao "Jeshini hakuna ajira ni wito nakujitoa kwa dhati unaweza kufa vitani hivyo natoa wito kwa wale wanaoingia Jeshini kwa Lengo la kutafuta Pesa nawashukuru Sana wanatanzania kwa Ushirikiano makubwa" LUTENI GEN.(Msaatafu)Paul Masao.
Katika historia ya jeshi hilo wapo wanawake wawili waliopata kuwa na vyeo vya brigedia general Tanzania nzima ambapo mmoja wao aliyestaafu hakusita kueleza safari yake ya mafanikio katika utumishi huo "Nimeanza kulitumikia jeshi la wananchi JWTZ Tangu nikiwa binti mdogo Sana Hadi hii Leo nimefikia kustaafu nawashukuru Sana Viongozi wangu kwa kunilea niwaambie tuu kuwa Jeshi Lina misingi ukiifuata utaheshimika".Brig.Jen.(Mstaafu)MARY HIKI.
Baada ya kustaafu kwa Brig jen Mary Hiki kwa sasa amebaki mwanamke mmoja Brig Jen Hawa Issa ambaye anajivunia kuwa Mtanzania pekee mwenye cheo hicho kwa upande wa wanawake katika jeshi
"Kwa upande wangu niseme tuu ntafuata mazuri kutoka kwa Afande anaestaafu hii leo natamani pia kufikia Katika siku kama hii ambayo Jeshi linakuaga kwa Heshima kubwa"Brig Jen Hawa Issa
Gwaride Hilo la heshima limehudhuriwa na Mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama Nchini Jenerali Venance Mabeyo akiwa pamoja na wakuu wa majeshi wastaafu waliopita Zikifanyika katika kambi ya Twalipo jijini Dar es salaam