Thursday , 23rd Oct , 2014

Nchi za Afrika Mashariki zashauriwa kubadili mifumo yake ya elimu ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.

Katibu  Mtendaji  wa  Baraza la Biashara la EAC Prf.  Mayunga Nkunya

Mwenyekiti wa  Baraza  la Biashara la nchi  wanachama wa  Jumuiya ya Afrika  Mashariki  Bw. Felexs  Mosha  amesema   jitihada  za  kukabiliana  na  tatizo  la  ajira  kwa  vijana     wakiwemo   wanaomaliza  vyuo  vikuu zitakuwa  na  mafanikio  kama  serikali  za  nchi  wanachama  zitakubali  kuwa  na mfumo  shirikishi   wa  elimu  na  unaozingatia  mahitaji  soko la  ajira   kwa  sasa.

Bw  Mosha  ameyasema  hayo    katika   mkutano wa  Baraza  hilo  la  biashara   na   Baraza la Vyuo Vikuu  la Afrika Mashariki,  Baraza la Biashara la Afrika Mashariki na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki, unaofanyika  Kigali, nchini  Rwanda..
Katibu  Mtendaji  wa  baraza  hilo  Prf.  Mayunga Nkunya  amesema  pamoja  na  changamoto zinazowakabili   wahitimu    wa   vyuo  vikuu  katika  nchi  za  Afrika  Mashariki  uchumguzi umeonesha  kuwa  wana  uwezo mkubwa  wa  kuleta mabadiliko   kama  mfumo uliopo  utabadilika.
 
Akizungumza  wakati   anafungua  mkutano  huo   waziri wa elimu wa Rwanda Prof. Silas Lwakabamba  amesema licha  ya  vyuo  vikuu  vya  EAC   kuzalisha wahitimu wanaokubalika katika soko la ajira   hawauziki kutokana na  kuwa na kujengwa  katika  mfumo   usiokidhi   soko   la  ajira la  sasa