Saturday , 18th Jul , 2020

Mtaalamu wa Soka kutoka East Africa Radio, Ibra Kasuga leo alikuwa na mahojiano maalum na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Wilfried Kidau kutazama maendeleo ya soka nchini tangu uongozi huo ulipoingia madarakani mwaka 2017.

Pamoja na mambo mengi ambayo Katibu Mkuu Kidau aliyafafanua ni pamoja na suala la faida ambayo itapatikana kwa kupunguza timu za Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kutoka 20 hadi 16 kuanzia msimu ujao, ambapo amesema klabu zitapata pesa nyingi kutoka kwa wadhamini.

"Klabu za ligi kuu hivi sasa zinapata takribani milioni 280 kwa msimu mzima kutoka kwa wadhamini mbalimbali wa ligi, hivyo msimu ujao zitaweza kunufaika zaidi kutokana na kupunguzwa timu hadi 16", amesema Wilfried Kidau.

Pia Katibu Mkuu, Wilfried Kidau amezungumzia suala la uwezekano wa kutumia waamuzi 6 katika mechi za ligi kuu kuanzia msimu ujao, ambapo amesema, "tunavyokwenda msimu ujao tunakwenda kuzalisha waamuzi vijana ambao wataweza kuchezesha wakiwa sita katika mchezo. Lakini tukiwa tunafikiria suala hilo kuna suala la fedha za uendeshaji hapo", ameongeza.

Kutazama ufafanuzi wote alioutoa Katibu Mkuu Kidau, tazama hapa