Tuesday , 21st Oct , 2014

Polisi nchini Uganda, wanaendesha uchunguzi juu ya tukio la kuchomwa moto kwa gari ya msanii Big Eye kutoka nchini Uganda, tukio lililotokea usiku wa kuamkia jana.

msanii wa muziki wa nchini Uganda Big Eye

Msanii huyu kupitia njia ya mtandao ameandika kwa masikitiko ujumbe akiwauliza wabaya wake ni jambo gani amewafanyia mpaka kufanyiwa kitendo hicho cha kinyama.

Gari ya msanii huyu iliyoungua ni aina ya Toyota Noah na tukio hili lilitokea katika eneo analoegeshea gari nyumbani kwake.