Tundu Lissu
Kuelekea Mkutano wa Baraza Kuu la chama na Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 29, Lissu amesema atahudhuria mkutano huo utaompitisha mgombea Urais wa chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2020.
Tundu Lissu ni mmoja wa watia nia waliojitokeza kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu, wengine ni wakiwemo, Mwenykiti wa chama, Freeman Mbowe, Mbunge Peter Msigwa na mwanasiasa Lazaro Nyalandu.
Tangu alipopelekwa nje ya nchi kwa matibabu tangu Septemba mwaka 2017, Lissu hakuwahi kurudi nchini na hiyo itakuwa ni mara ya kwanza baada ya tukio la kushambuliwa na watu wasiojulikana.