
Msanii Madee
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Madee amesema siasa zina maneno mengi, ambayo unatakiwa uwe mjanja ili uweze kuwashinda watu ili ukitaka ugombee ndiyo upewe.
"Napenda kuingalia siasa na kuisoma ila siwezi kuifanya, kwa sababu ina maneno mengi ambayo unatakiwa uwe mjanja ili uweze kushinda, siasa ni maisha ila sijawahi kufikiria wala kuwaza, japo natumiwa sana ujumbe na maombi na viongozi wa vyama tofauti tofauti kwamba wanipe nafasi niongoze Ubungo au Udiwani Manzese, na wanatamani niingie kwenye siasa" ameeleza Madee.
Zaidi tazama kwenye video hapa chini.