Tuesday , 28th Apr , 2020

Mdogo wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anayefahamika kwa kwa jina la Bernard Lowassa, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Aghakhan jijini Dar es salaam.

Edrward Lowassa na mdogo wake ambaye ni marehemu Bernard Lowassa

Mtoto wa Waziri Mkuu huyo Mstaafu Fred Lowassa amethibitisha hayo wakati akizungumza Mwandishi wetu wa EATV na EA Radio Digital, Sangu Joseph, ambapo amesema kwa sasa familia inaenda kukutana.

Fred amesema kuwa "ni kweli ndugu yetu Bernard lowassa amefariki yeye ni Baba yangu mdogo, na alikuwa amelazwa Aga Khan na hapa familia tunaenda hospitalini kwa ajili ya kukutana."

Kuhusiana hali ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa baada ya kupokea taarifa ya msiba Fred amesema "Mzee amepata mshtuko lakini yuko salama anaendelea vizuri

"Kwenye suala hili la Barakoa, kuna NGO's ziliomba kutengeneza barakoa ili kusaidia Watanzania, lakini sasa wanauza kwa bei ya 2500 - 3000, si wangesema wanataka kupata faida" - Innocent Bashungwa - Waziri wa Viwanda na Biashara.