Friday , 24th Apr , 2020

Mmoja wa wasanii ambaye ametoka Kings Music Records Official Cheed, amefunguka suala ambalo linazungumziwa kwa sasa kuhusu kuhamia lebo ya Konde Gang, ambayo ipo chini ya msanii Harmonize.

Msanii Cheed

 

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, amesema suala hilo halina ukweli wowote na hata yeye analisikia mitandaoni japo kwa sasa hivi anashambuliwa kwa matusi baada ya kutoka kwa Alikiba.

"Hakuna mtu ambaye ametushika akili tutoke Kings Music ni stori ambazo zinatengenezwa kutokana na hili tukio, suala la sisi kwenda Konde Gang halina ukweli wowote japo hata mimi nalisikia kwenye mitandao, lakini kwa sasa hakuna ukweli juu ya hilo, na sasa hivi nashambuliwa kwa kutukanwa sana hadi nazima simu ila mimi nachukulia kama changamoto" ameeleza Cheed.

Mahojiano kamili tazama kwenye video hapa chini.