
Askofu wa Dayosisi ya Karagwe, Dkt Benson Bagonza.
Hayo ameyabainisha kupitia barua yake ya kusitisha mikusanyiko yote ya kiibada, kuanzia Aprili 26 kwa Dayosisi ya Karagwe, kutokana na hali ya mwenendo wa maambukizi ya Virusi vya Corona nchini kuendelea kuongezeka.
"Tuko vitani na adui Corona, usahihi na mazoea ni sehemu ya tatizo, binadamu wote ni sawa tunaona binadamu wengine duniani wanakufa kwa wingi, kwahiyo kutochukua hatua ni sawa na kusema sisi si binadamu kama wanaokufa" ameeleza Askofu Dkt Bagonza.
Aidha Dkt Bagonza amesema kuwa hizi ni nyakati zisizo za kwaida na kwamba kama hatuwezi kuwa suluhisho la tatizo, basi sisi ni sehemu ya tatizo na katikati hapakaliki kwa amani.