Tuesday , 14th Apr , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amesema kuwa hana mpango wowote wa kugombea Ubunge wa Jimbo la Hai, kwa kuwa imani aliyopewa na Rais Magufuli juu ya kuwatumikia wananchi wake ni kubwa na ataendelea kuifanya kwa uadilifu mkubwa.

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya.

Hayo ameyabainisha wakati alipofanya mazungumzo maalum na EATV&EA Radio Digital, ambapo mwandishi wake alimhoji kama anayo nia ya kumpiku Mbunge wa Jimbo la Hai Freeman Mbowe.

"Hapana sina mpango huo, natamani kuendelea kuwahudumia wananchi  kwa heshima aliyonipa Mheshimiwa Rais inanitosha, kuhakikisha wananchi hawa wanapata haki zao kwa sababu ndiyo matamanio makubwa ya Rais Magufuli na kazi hii naifanya kwa uaminifu na uadilifu mkubwa, sijamaliza hii kazi aliyonipa sasa Ubunge wa nini mimi" amesema Sabaya.