Friday , 10th Oct , 2014

Serikali imesema itaboresha Miundo mbinu ya vyuo vikuu vya Ualimu nchini hasa katika kufundisha Masomo ya Sayansi ili kuweza kuboresha ufundishaji wa Masomo hayo kuanzia Shule za Msingi mpaka sekondari kwa Ufanisi.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Jenista Mhagama.

Akiongea Mjini Morogoro Mbele ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jana Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bi. Jenista Mhagama amesema ili kuweza kupata matokeo makubwa sasa BRN serikali haina budi kuboresha vyuo hivyo kukuza masomo ya sayansi.

Bi. Jenista ameongeza kuwa mradi huo utawawezesha walimu kufundisha masomo ya sayansi na Kuongeza kuwa hakuna njia mbadala ya kuweza kukuza somo hilo zaidi ya kuwapa ujuzi walimu kufundisha mada ngumu zaidi ili kuweza kukuza masomo hayo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda amewataka walimu wajifunze kwa vitendo zaidi kwa kile wanachokifundisha ili wawe mfano bora kwa wanafunzi wanaofundisha kuzingatia masomo hayo.