Friday , 13th Mar , 2020

Aliyekuwa mkali wa miondoko ya muziki wa Taarab Mzee Yusuph, amesema anatafuta nauli ya kurudi kwenye muziki ambapo alitangaza kuacha  kufanya  kazi hiyo miaka minne iliyopita na kuanza kumtumikia Mungu.

Mzee Yussuf

Mzee Yusuph ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram,  "Wakati naanza mziki huu wa kidunia, nilikua nina mori kuliko mmasai, ila muda ulipokwenda  mori ikapungua kisha nikaacha kwa kuwa nilihisi sioni sababu ya kuendelea, cha kushangaza sasa hivi nina hamu ya kuimba balaa, nataka niimbe mpaka nigaregare mwaka huu" ameandika Mzee Ysuph.

Sasa Kupitia EATV & EA Radio Digital Mzee Yusuph amefunguka na kusema atarudi kuimba sana ila bado hajajua ataimba muziki wa aina gani kama ni singeli au taarab na sasa hivi anatafuta nauli ya kurudi mjini.

"Nitaimba sana nikija mjini ila sijajua ni muziki gani kama ni kisengeli, kiduku au Taarab, nimeacha kuimba miaka minne pengo lipo na ndiyo wakati wa kuzibwa sasa, kuimbwa hatujakatazwa kwa sasa natafuta nauli ya kurudi mjini" amesema Mzee Yusuph.