Friday , 13th Mar , 2020

Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, pamoja na Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, kwa pamoja wameeleza ni kwa namna gani walivyolazimishwa kujisaidia kwenye ndoo chafu gerezani ili hali hawakuwa wamebanwa haja.

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Wakizungumza leo Machi 13, 2020 mara baada ya kutoka gerezani, Mbunge Mchungaji Peter Msigwa yeye amesema kuwa wao walivuliwa nguo ili hali siyo wahalifu na kupanga foleni.

"Tunapita kwenye njia iliyopambwa maua, hii njia ndiyo tumeiendea magereza tukiwa na shangwe, Heche hajasema vizuri, tumepangwa tukiwa uchi wa mnyama, sisi sio wezi tumetoka mahabusu wote tukiwa uchi, tumekalia ndoo chafu na kulazimishwa kwamba tujisaidie" amesema Msigwa.

Kwa upande wake Mbunge Heche ameeleza kuwa, yeye alikuwa tayari kwa kufungwa na si kulipa faini,"Mimi nilijiandaa kufungwa na siyo kupigwa faini na nilikuwa sawasawa na sitapigia mtu yeyote magoti kwa kitisho cha gereza ama kuniua".