Haruna Niyonzima
Akiwa katika moja ya programu ya mazoezi, Haruna amesema kuwa anaamini mchezo huo utakuw mgumu sana kutokana na historia ya timu zenyewe na mashabiki wao lakini wao kama Yanga wanayo nafasi ya kushinda.
"Nakumbuka mchezo wa mwisho uliisha kwa sare ya mabao 2-2, lakini kwa hii inayofuata itakuwa ni ngumu na nzuri iwe kwa Yanga au Simba kwa sababu kila timu itataka kuonesha kuwa wao ni wazuri", amesema Niyonzima.
"Siwezi kusema sehemu gani itaamua matokeo, mimi naizungumzia timu yangu ya Yanga kwamba tukijipanga vizuri na kufanya mwalimu anachokihitaji na Mungu akitujaalia tutashinda", ameongeza.
Joto la mchezo huo limeanza kupanda zimebakia takribani siku 12, huku kila upande ukijidai kuwa unataka kuonesha uwezo wake. Simba ipo kileleni mwa ligi kwa pointi 62 huku Yanga ikiwa katika nafasi ya nne kwa pointi 41.


