Saturday , 28th Dec , 2019

Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera amethibitisha kuwa ameishtaki klabu hiyo katika shirikisho la soka duniani (FIFA) na kwa mujibu wa kanuni alivyofuatilia ana uhakika kuwa watamlipa mara mbili ya pesa anazodai kutokana na usumbufu aliopata.

Kocha Mwinyi Zahera

Zahera amesema ameshafuata taratibu zote kwani anajua pesa yake alitakiwa kulipwa mapema baada tu ya kufukuzwa.

'Wanasema hawana hela sasa tutajua, maana makocha wote waliofukuzwa wakiwemo wale wa Simba na Azam FC walilipwa pesa zao siku hiyo hiyo maana huwezi kufanya maamuzi bila kujua utatoa wapi pesa', amesema Zahera.

Zaidi msikilize hapa akieleza zaidi.