Saturday , 28th Dec , 2019

Naibu Waziri wa Utalii, Costantine Kanyasu, amesema baada ya Faru Fausta kufariki kama Wizara watashirikiana na baadhi ya wanasayansi ili kuangalia namna ya kuhifadhi mwili wa mnyama huyo ili aendelee kuwa ambapo Watalii wataendelea kuja kumuona kama kivutio cha utalii.

Faru Fausta

Naibu Waziri Kanyasu amesema moja ya sababu ya kifo cha Fausta ni uzee ambapo kwa sasa ana miaka zaidi 56, huku akiwa na watoto na wajukuu wengi.

Kanyasu amesema kuwa " Ni kweli Faru Fausta amefariki Dunia tena akiwa na miaka 56 na amefariki sababu ya kuishi muda mrefu"

"Kama Wizara tunashirikiana na wanasayansi ili kuangalia namna ya kumuhifadhi huyu Faru kwa kuwa ameingizia Taifa pesa nyingi sana." amesema Kanyasu