
Dr. Kigwangalla na baadhi ya wasanii wa Bongo Movie kwenye matembezi ya kampeni ya Twenzetu Kinature.
Kampeni hiyo imelenga pia kuhamasisha Watanzania kutembelea maeneo mbalimbali ya historia na maeneo ya misitu iliyopo Tanzania kujionea uoto wa asili na viumbe wanaopatikana humo ambao hawapatikani sehemu nyingine yoyote Duniani.
Maeneo yaliotembelewa ni pamoja Ngome kongwe na eneo la Kaole katika wilaya ya Bagamoyo, Tongoni ambapo pana masalia ya majengo na sanaa nyingi za mji wa kale katika mkoa wa Tanga. Maeneo mengine ni mapango maarufu ya Amboni pamoja na Misitu ya hifadhi wa mazingira asilia wa Amani uliopo wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
Watanzania wanahasishwa hasa katika kipindi hiki cha sikukuu, kutembelea maeneo mbalimbali kwa mapumziko pamoja na kuibeba kampeni iliyopewa jina la Twenzetu Kinature.
Hizi ni baadhi ya picha ya safari hiyo.