
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Mbowe ametoa kauli hiyo katika Mkutano Mkuu wa chama hicho, wakati wakiendelea na zoezi la uchaguzi na uteuzi wa viongozi wake mbalimbali na kuwataka vijana kuwa makini na majibu yao.
"Wajibu wetu kama CHADEMA ni kukipenda chama chetu kwa wivu mkubwa, niwahase vijana mnaochipukia kwenye siasa, mimi ni mtu mwepesi sana wa kukubali ushauri, mimi siri yangu moja kwenye uongozi wa siasa mimi ni mwepesi sana wa kusikiliza, hakuna yeyote anayekuja kwangu sijamsikiliza" amesema Mbowe.
Aidha Mbowe aliendelea kusema, "Nashambuliwa sana, natukanwa sana lakini mara nyingi nakaa kimya kwa sababu najua kukaa kimya ni jibu".
"Nashambuliwa sana, natukanwa sana lakini mara nyingi nakaa kimya kwa sababu najua kukaa kimya ni silaha" - @freemanmbowetz pic.twitter.com/cMCowgwQfh
— East Africa Radio (@earadiofm) December 20, 2019