
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mtemi Msafiri.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa ufunguzi wa kambi okozi kwa ajili ya mabinti, wanaokimbia ukeketaji na kukimbilia Katika kambi ya ATFGM Masanga.
"Sheria zipo na lazima tuzisimamie, niwaambie nimepata habari kuna Mtendaji mmoja wa Serikali amekeketa watoto wake na tumemfuata bahati mbaya hatukuwakuta watoto wake, tunasubiri wakirudi tu tunamkamata" amesema DC Msafiri.
Aidha Msafiri ameongeza kuwa "Niseme tu mila zozote zinazoenda kinyume na sheria za nchi, lazima tuzisimamishe, kama kuna kiongozi yeyote wa Serikali, anashiriki mambo hayo mnieleze naenda kumkamata".
#HABARI Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mtemi Msafiri ametoa onyo, kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao wanajihusisha na suala la ukeketaji. pic.twitter.com/w58VI9LBui
— East Africa Radio (@earadiofm) December 13, 2019