
Kushoto pichani ni Wema Sepetu akiwa na Martin Kadinda.
Martin Kadinda amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuwepo na taarifa kuwa ule ukaribu wao wa mwanzo umepungua ambapo ameeleza,
"Hayo ni mawazo binafsi ukiangalia kwenye mitandao ya kijamii nipo na Wema Sepetu, Mimi mwenyewe kwangu nilikuwa naye ni kwamba nimeamua tu kumuweka Wema nyuma sio mbele kama ilivyokuwa kwa sababu mimi nina biashara natakiwa kuifanya na yeye anatakiwa aendeleze maisha yake" amesema Martin Kadinda.
Aidha Martin Kadinda ameendelea kusema "Nimejaribu kutofautisha urafiki na kazi kwa sababu zamani labda nilimpa asilimia 80 ya maisha yangu lakini sasa hivi nimeamua kufanya 50 kwa 50 ila sio kwamba kuna utofauti tupo sawa" ameongeza
Pia akizungumzia suala la Wema Sepetu kutojenga nyumba amesema, hayo ni mambo binafsi ya mtu hakuna aliye na ushahidi kama amejenga au hajajenga, kila mtu anakuwa na mipango au mawazo yake ya kufanya.