Rais wa TFF Wallace Karia (kushoto) na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela (kulia).
Akiongea na EATV&Radio Digital, Mongela amesema kuwa wakazi wa kanda ya ziwa wanapenda mpira na ndio maana walijaza uwanja wa CCM Kirumba hivyo wanatakiwa waendelee kupata michezo mikubwa hata ya kitaifa.
'Uamuzi wa Yanga kuleta mechi Mwanza ni wa busara sana na uongozi wa Yanga umeona watu wamefurika, kwahiyo tujenge haya mazoea, na pia nimewaambia viongozi wa TFF waliokuwepo hapa Mwanza kuwa watuletee hata mechi ya timu ya taifa sisi tutaandaa', amesema Mongela.
Kwa upande mwingine mkuu huyo wa mkoa ameweka wazi kuwa wangetamani mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2021 nchini Cameroon dhidi ya Tunisia utakaopigwa mwakani ukachezwe kwenye uwanja wa CCM Kirumba.


