Sunday , 27th Oct , 2019

Mwanariadha Alphonce Simbu amefanikiwa kupeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya majeshi ya Dunia na kujinyakulia medali ya Fedha (Silver).

Mwanariadha Alphonce Simbu

Mwanariadha huyo 'private' akiwakilisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, alimaliza baada kukimbia saa 2:11:16 huku akiwaahinda wakimbiaji wengne 95 kutoka nchi zaidi ya 30.

Katika mbio hizo mshindi wa Kwanza ni Luche Sumi kutoja Bahrain aliyekimbia 2:08:28, mshindi wa tatu ni mwanariadha kutoka Rwanda John Hakizimana akiyekimbia kwa karibu nyuma ya Simbu kwa 2:11:19.