Wakandarasi hao kutoka kampuni ya CHICCO na Nyanza, wamekamatwa leo Oktoba 24, 2019 kwa makosa ya kushindwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa Barabara ya Kivule pamoja na mradi wa ujenzi wa mto Ng'ombe, Jijini humo.
Kwa mujibu wa Makonda, Mkandarasi wa Kampuni ya CHICCO, amekamatwa kwa kushindwa kutekeleza mradi wa Mto wa Ng'ombe, ambao licha ya kuwa amekwishalipwa hela kiasi cha Shilingi bilioni 4.8, lakini hadi sasa hakuna chochote alichokifanya, huku wananchi wakiendelea kuteseka na kero ya mafuriko.
Kwa upande wa Kampuni ya Nyanza, mkandarasi huyo anadaiwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Kivule pamoja na Daraja, licha ya Kupokea fedha zaidi ya Shilingi Milioni 800, jambo linalopelekea wakazi wa Kivule kuteseka na kero ya ubovu wa Barabara.

