Adele na aliyekuwa mume wake
Katika rekodi za mahakama zilizotoka hivi karibuni zimeonesha Adele akifuatilia taratibu kadhaa za kudai talaka, ombi aliloliwasilisha tangu Alhamisi wiki iliyopita huku chanzo cha utengano wao kikiwa bado hakifahamiki.
Adele na Simon walianza kutoka pamoja kimapenzi mwaka 2011 na mwaka 2012, walifanikiwa kupata mtoto wa kiume, baada ya hapo walifunga harusi ya siri na hakuna kilichoendelea kufahamika kuhusu maisha yao kwa pamoja.
Mara ya mwisho kuonekana pamoja ilikuwa ni katika tamasha la mwanamuziki Elton John huko Los Angels, Marekani na walifika wakiwa pamoja huku wakionekana kuwa na furaha lakini zaidi ya hapo hawajawahi kuonekana tena.
Mara ya mwisho Adele kuachia albam ilikuwa mwaka 2015 iliyopewa jina la “25”, ikiwa na mjumuiko wa ngoma zilizofanya vizuri sana kama Hello, When We Were Young, Send My Love (To Your New Lover) na nyinginezo nyingi. Zaidi ya hapo hakuna kazi nyingine yoyote ambayo ameachia.
Taarifa kadhaa zinasema huenda kabla ya mwaka 2019 haujaisha albamu mpya kutoka kwa Adele inaweza kuachiwa huku mwezi Desemba ukitajwa huenda ukawa ndiyo wa maajabu hayo kutokea kwa mashabiki wote wa Adele.
