Mbunge Mtolea amesema kuwa, "mimi niko Dodoma kwenye vikao vya Bunge kwa hiyo siwezi kulisema kwa sasa ila kila jambo linaloendelea na mimi nimeshiriki na ninaliunga mkono, kwa sababu mimi ni mmoja wa Wajumbe wa Baraza la Jiji na kila kinachoendelea mimi nipo."
"Kuhusu kuzungumzia kiundani kwa sasa siwezi kwa sababu nimeondoka wiki 2 zilizopita, ila kila jambo linaloendelea na mimi nipo ndani yake kwa sababu ni mjumbe wa Baraza hilo kupitia CCM," amesema Mtolea
Mapema jana akizungumzia tukio hilo, Meya wa Temeke Abdallah Chaulembo, alisema ni kweli wamefikisha malalamiko hayo na wanatarajia leo Septemba 13, 2019 kupokea majibu ya Meya Mwita.
Juhudi za kumpata Meya Isaya Mwita kwaajili ya ufafanuzi kwa upande wake bado zinaendelea.
