Thursday , 29th Aug , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, amewataka wakazi wa Mkoa huo kubadili namna mpya ya nyumba za kuishi, kwa kutoishi kwenye nyumba za kuwekeza kwa kwa matope na nyasi, badala yake waaanze kujenga nyumba za matofari na kuweka mabati.

Zambi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakazi waishio eneo la Mlandege, Kata ya Nachingwea Manispaa ya Lindi.

Akizungumza na wananchi hao, Zambi amewataka kutojenga nyumba zao kwa kutumia tope na nyasi, badala yake wajenge kwa kutumia matofari na kuezeka Bati.

"Ndugu zangu hapa ni Mjini tena ni Manispaa, inatakiwa majengo yake yawe na hadhi,sawa na Jina lenyewe ninawaomba watu ambao mmepewa viwanja kwenye maeneo hayo mjenge nyumba ambazo, zinaendana na hadhi ya mjini bila hivyo, ukishindwa tutawapatia watu wenye uwezo."amesema Zambi.

Aidha amesema mtu atakayeshindwa kutekeleza hilo ni atatakiwa kuondoka na kwenda kuishi Kijijini na kuwapisha wenye uwezo wa kujenga nyumba za kisasa.