Thursday , 8th Aug , 2019

Mkuu wa Idara ya Viwanda na ushindani wa Jumuiya ya SADC, Johansein Rutaihwa, amesema wanaendelea kuhakikikish nchi zote 16 wanachama wa SADC zinasaidiwa kuhakikisha zinafikia ukuaji wa uchumi kwa asilimia 7.

Mkuu wa Idara ya Viwanda na ushindani wa Jumuiya ya SADC, Johansein Rutaihwa.

Rutaihwa ameyabainisha hayo leo kupitia East Africa Breakfast ya East Africa Radio, ambapo ameeleza mipango pamoja na utendaji kazi wa Jumuiya hiyo kwa nchi wanachama wake.

Kwa upande mwingine Rutaihwa ameeleza kuwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika inafanyakazi kwa ukaribu na Jumuiya nyingine ili kuhakikisha kwa pamoja bara la Afrika linapiga hatua.

Aidha amebainisha kuwa katika kuelekea mkutano huo wa wakuu wa nchi hizo ambao utafanyika Agosti 17-18 mwaka huu, lakini shughuli mbalimbali ikiwemo maonyesho ya biashara na viwanda kwa nchi wanachama yanaendelea.