
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kwa mwaka huu tamasha hilo litakuwa la aina yake.
"Tukio letu la wiki ya Simba limeigwa maeneo mbalimbali, lakini sisi tutataka kulifanya kwa ubora zaidi, na kauli mbiu yetu itaitwa 'Iga Ufe, This is Next Level #10 Years Anniversary Of Simba Wiki" amesema Manara.
Awali Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori, amesema wiki ya Simba imetawaliwa na matukio mbalimbali ikiwemo utoaji damu, pamoja kutoa misaada kwenye Hospitali mbalimbali nchini.
"Tarehe 3 Agosti, nchi nzima iwe nyekundu, twende kwenye Mahospitali tukawasaidie watu wasiokuwa na uwezo. Mungu ametujaalia mwaka jana tumefanya vizuri sana inabidi mwaka huu tupate baraka za watu hawa wenye uhitaji." amesema Magori.