
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Anna Henga
Akitoa tamko kwa niaba ya mtandao huo, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC Anna Henga, amesema vitendo hivyo ni vya udhalilishaji wa utu wa mwanamke, ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na kuingilia uhuru wa faragha.
"Katika hali isiyokuwa ya kawaida picha za wanawake hao zilisambaa mitandaoni na imethibitika kwamba zilipigwa na maofisa wa polisi wa kituo cha Mburahati na tuliongea na Mkuu wa kituo hicho na akathibitisha kwa kusema zilipigwa kwa manufaa ya kikazi lakini tukaziona kwenye mitandao'' Amesema Anna Henga.
Aidha mtandao huo umetoa wito kwa Jeshi la polisi, kuwachukulia hatua za kinidhamu wahusika wa kitendo hicho ili kulinda utu wa mwanamke na watuhumiwa wa makosa ya jinai.
Ameongeza kwamba mtandao huo hautosita kuchukua sheria, ikiwemo kufungua mashtaka kwa wahusika wa tukio hilo.
#VIDEO Mkurugenzi wa @humanrightstz Anna Henga kwa niaba ya Mtandao wa kupinga Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) ameeleza kusikitishwa na vitendo vya kusambazwa kwa picha zinazoonesha wanawake wanne, waliokuwa wakituhumiwa na kushikiliwa katika kituo cha polisi cha Mburahati Dar. pic.twitter.com/CY9bbbZBgb
— East Africa TV (@eastafricatv) July 26, 2019