Friday , 12th Jul , 2019

Barcelona imefanikiwa imefanikiwa kumsajili Antoine Griezmann baada ya kuilipa Atletico Madrid Euro milioni 120 kwaajili ya 'buyout clause'. 

Antoine Griezmann

Griezmann atasaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Barcelona utakaomalizika Juni 30, 2024. Mkataba huo utakuwa na 'buyout clause' ya Euro milioni 800.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa, amejiunga na Barcelona ikiwa ni kutimiza mpango wake alioutangaza mwisho wa msimu wa 2018/19 ambapo aliweka wazi kuwa hataendelea na Atletico Madrid.

Barcelona na Atletico Madrid zimefikia makubaliano hayo baada ya kuanza mazungumzo Julai 1, 2019 ambapo kipenegele cha kuruhusu Antoine aondoke endapo timu itafikia dau la Euro milioni 120 kilianza kufanyakazi.

Griezmann alianza kufanya vizuri akiwa na miaka 14 ndani ya klabu ya watoto ya Real Sociedad kati ya mwaka 2005 na 2009 na baadaye kujiunga na timu ya wakubwa akiwa na miaka 18 kuanzia 2009 hadi 2014 alijiunga na Atletico Madrid.