
Mwinyi Zahera (katikati)
Dismas amesema soka ni mchezo wa kiungwana, haiwezekani wengine waugeuze kuwa sehemu ya uchochezi na ubaguzi kitu ambacho sio sawa hata Simba waliwahi kufanya hivyo msimu uliopita ambapo kocha wao msaidizi kwa wakati huo Masoud Djuma pamoja na Haruna Niyonzima waliwatembelea Rayon Sports walipokuja kucheza na Yanga.
''Kauli za kichochezi dhidi ya kocha Zahera Mwinyi, wana Yanga wote tuamini kuwa jambo lolote baya litakalo mpata kocha wetu basi uongozi wa Simba unahusika, ama la wajitokeze hadharani kukanusha au kuzikemea kauli hizo'', amesema Dismas.
Mapema jana msemaji wa Simba Haji Manara alimtuhumu kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kuwa aliaga anaondoka nchini kwenda DR Congo lakini yupo na AS Vita Dar na wala hajaenda Iringa ambako Yanga itacheza na Lipuli FC leo.
Simba leo inacheza mchezo wake wa mwisho kundi D, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita kwenye uwanja wa taifa kuanzia saa 1:00 usiku ambapo inahitaji ushindi ili ifuzu robo fainali.