Monday , 18th Aug , 2014

Tamasha kubwa la muziki, Kilimanjaro Music Tour 2014 limeweza kwa mara nyingine kuweka rekodi ya kumwaga burudani kwa wakazi wa Dodoma, ambapo siku ya Jumamosi timu ya mastaa wakali kabisa wameweza kuwasha moto katika uwanja cha Jamhuri.

Msanii Christian Bella akitumbuiza katika tamasha la Kili Music Tour Dodoma

Mbali na burudani nyingine kubwa, Kivutio cha aina yake katika onesho hili zima ni pale wasanii MwanaFA, mtoto wa nyumbani Ben Pol, Christian Bella, Mwasiti na kundi la weusi walipokuwa wanatumbuiza juu ya jukwaa.

Hivi ndivyo Dodoma ilivyo nyeshewa na mvua ya Burudani, mashambulizi yanaelekea Kigoma mwishoni mwa wiki hii, Kilimanjaro Music Tour 2014, Zungusha Kikwetu Kwetu.